27 Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,
28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.
29 Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
30 Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.
31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.
32 Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
33 Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.
35 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.
36 Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.
38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Inaoneka kwa wakristo wengi kuwa ni ngumu kufuata maagizo haya lakini mpendwa ndugu yangu napendanikupe habari hii. Mungu anachotaka kwako ni roho iliyopondeka katika kuamini sharia na maagizo yake na mengine tunayaweza tukiwa ndani yake. maana ni yeye anayetushindia
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.