Tatizo ni lile lile, mwingine anafunga na kuomba, na mwingine anarudi nyuma kiimani. Tatizo ni lile lile mwingine anafikiria ni namna gani alitatue mwingine, anaamua kujiua.
"Kinachowafanya watu watofautiane sio kwa sababu wengine hawapitii matatizo, na wengine wanapatwa na matatizo makubwa zaidi, bali ni namna wanavyokabiliana na hayo matatizo."
Mtu aliyegundua nukta nundu (braille) herufi za vipofu; alikuwa ni kipofu aliyepata upofu kutoka na kujichoma kwa bahati mbaya jichoni na kifaa chenye ncha kali ambacho baba yake alikuwa anakitumia kutobolea ngozi, alipokuwa na umri wa miaka mitatu. Baadaye jicho moja lililobaki likaathiriwa na tatizo lile, hivyo hilo nalo likapata upofu. Kwa hiyo akawa kipofu wa macho yote mawili.
Lakini tatizo la upofu alilo kuwa nalo halikuwafanya wazazi wake wamkatie tamaa, wala yeye mwenyewe kukata tamaa; bali walimpeleka shule.
Kutokana na upofu alionao, alitafuta njia ya kujisaidia mwenyewe na vipofu wengine kuweza kusoma maandishi. Hivyo aligundua nukta nundu/herufi za vipofu (breilla). Upofu wake ulimpelekea kugundua nukta nundu ambazo leo hii ndio zinatumiwa na vipofu kusoma.
Ukisikia kipofu ana PHD, ujue ni kutokana na mtu kipofu aliyeitwa Breilla, aliyegundua hizo nukta nundu.
*UPOFU WAKE NDIO CHANZO CHA KUGUNDULIWA KWA NUKTA NUNDU AMBAZO VIPOFU WANAZITUMIA KUSOMEA.*
Kuna matatizo mengine Mungu anaruhusu upitie ili uwe suluhisho la matatizo ya watu wengine. Hivyo usimlaumu, Mungu, usiwalaumu watu, wala usikate tamaa kwa changomoto unazopitia. Kwani inawezekana Mungu ameruhusu upitie hayo ili uwe jibu la matatizo ya watu.
*NAKUONA UKIFANYIKA JIBU LA MATATIZO YA WATU KAMA ILIVYOKUWA KWA YUSUFU KUTOKANA NA CHANGAMOTO UNAZOPITIA !!*
*NI MAOMBI YANGU NA DUA YANGU KWAKO, CHANGAMOTO UNAZOPITIA ZISIKUFANYE UMWACHE MUNGU, BALI ZIKUSOGEZE ZAIDI KARIBU NA YEYE !!*
*MUNGU WANGU AKUBARIKI.*
*Mchungaji na Mwalimu Gibson Gondwe.*
_*Ukitaka masomo yangu kwa njia ya whatsApp unaweza kunitumia namba yako inbox au ukaituma kupitia namba yangu hapo chini.*_
Kuna matatizo mengine Mungu anaruhusu upitie ili uwe suluhisho la matatizo ya watu wengine. Hivyo usimlaumu, Mungu, usiwalaumu watu, wala usikate tamaa kwa changomoto unazopitia. Kwani inawezekana Mungu ameruhusu upitie hayo ili uwe jibu la matatizo ya watu.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.