NAMNA YA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU.
Kumpokea Roho Mtakatifu kupo hivi:
Kumpokea Roho Mtakatifu huja tu baada ya mtu KUISIKIA INJILI, KUIAMINI INJILI, KUMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO WEWE MWENYEWE, KUTUBU DHAMBI, na KUMKABIDHI YESU ATAWALE MAISHA YAKO KAMA JINSI APENDAVYO YEYE.
Hiyo ndiyo kanuni ya kumpokea Roho Mtakatifu. Jambo hili halihitaji wewe kujitaabisha au kuanzisha maombi ya kufunga ili Roho Mtakatifu aje kwako. Si hivyo. Kumpokea Roho Mtakatifu huja AUTOMATICALLY kwa njia ya imani bila hata wewe kumbembeleza. Si lazima mtu aweke mikono kichwani mwako ili wewe ujazwe Roho Mtakatifu; wala si lazima mchungaji wako akuombee ili wewe ujazwe Roho Mtakatifu. Japokuwa wapo watu ambao walimpokea Roho Mtakatifu baada ya kuombewa na kuwekewa mikono juu ya vichwa vyao (Mdo 8:17) lakini hiyo SIO KANUNI ambayo ili mtu ampokee Roho Mtakatifu ni lazima afanyiwe hivyo. Huo ni ufunuo tu ambao walipewa kwa wakati huo, lakini sio kanuni ya kujazwa Roho Mtakatifu. Kamwe mafundisho ya Yesu hayatuambii kuwa kumpokea Roho Mtakatifu kunatokana na maombi ya kufunga kwa siku kadhaa. La hasha! Sivyo. Bali kumpokea Roho Mtakatifu huja kwa njia ya IMANI kwa mtu aliyeoshwa dhambi zake kwa damu ya Yesu Kristo. Ni lazima wewe uwe mtakatifu hapo ndipo Roho Mtakatifu atakaa ndani yako. Namna pekee ya kumpokea Roho Mtakatifu ni kumkiri Yesu awe Bwana na Mwokozi wako, pamoja na kuoshwa dhambi zako kwa damu ya Yesu.
Inawezekana hapa hujaelewa, hebu nikufafanulie hivi:
Je! Bwana Yesu aliwawekea mikono wanafunzi Wake ili wampokee Roho Mtakatifu? Je! Yesu alisemaje? Yesu alisema:
Je! Bwana Yesu aliwawekea mikono wanafunzi Wake ili wampokee Roho Mtakatifu? Je! Yesu alisemaje? Yesu alisema:
"...Pokeeni Roho Mtakatifu." ~ YOHANA 20:22.
Ni hivyo tu; na kweli wote walimpokea Roho Mtakatifu (MATENDO 2:4).
Je! Mtume Petro aliweka mikono juu ya Kornelio na juu ya watu wa nyumbani mwake ili wampokee Roho Mtakatifu? Je! Mtume Petro aliwaombea watu hao ili Roho Mtakatifu awashukie?
HAPANA. Bali Biblia inasema kwamba:
"Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno." ~ MATENDO 10:44.
Yeye Mtume Petro alikuwa bize akihubiri, watu wale walipoamini na kuweka tayari mioyo yao kwa ajili ya kumpokea Yesu, ndipo Roho Mtakatifu akashuka na kuweka makao Yake ndani yao. Roho Mtakatifu huweka makao Yake mahali ambapo ndani yake kuna CHAPA YA YESU. Kamwe hakuna mchungaji wala mtumishi ye yote yule wa Mungu awezaye kukuombea ujazwe Roho Mtakatifu endapo kama wewe HAUJAMKIRI YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO. Roho Mtakatifu haamrishwi na mtu kwamba INGIA KWA HUYO au YULE. Yeye Mwenyewe anaingia pale palipotakaswa kwa damu ya Yesu. Hauwezi kumlazimisha bali Yeye anaingia pale ambapo ni patakatifu tu. Kubatizwa au kutobatizwa si hoja Kwake, bali Yeye huutazama kwanza moyo wako kama Yesu ameshaweka makao Yake ndani yako, ndipo na Yeye Roho Mtakatifu huja na kuingia ndani yako. Wapo watu waliompokea Roho Mtakatifu kabla ya kubatizwa, na pia wapo watu waliompokea Roho Mtakatifu baada ya kubatizwa.
Kitu ambacho kinakuwa kizingiti kwa watu wasijazwe Roho Mtakatifu ni KUTOKUAMINI pamoja na DHAMBI kwa ujumla.
Je! Utajuaje kwamba umejazwa Roho Mtakatifu?
Utajua kwamba umejazwa Roho Mtakatifu kwa sababu maisha yako yatabadirika kimwili na kiroho pia.
KWANZA:
Utaona ipo nguvu ndani yako ambayo inakuamrisha ujitenge na dhambi. Kila kilicho dhambi utakatazwa usikifanye; utasikia sauti au nguvu kutoka ndani yako inayokushuhudia kwamba hicho si halali kwako kufanya.
PILI:
Utapata nguvu na hamu ya kujifunza neno la Mungu. Yawezekana hapo awali ulikuwa hauwezi kuomba kwa muda mrefu, au yawezekana ulikuwa haupendi kusikiliza mahubiri, au yawezekana ulikuwa haupendi uhudhulia ibada, au yawezekana ulikuwa haupendi kusoma na kujifunza neno la Mungu; lakini pindi tu Roho Mtakatifu awekapo makao ndani yako utajikuta automatically unampenda Mungu na kupenda kujifunza neno Lake.
TATU:
Utapata nguvu na ujasiri wa kulihubiri neno la Mungu. Katika kuhubiri ni lazima unawafundisha watu wawe wanafunzi wa Yesu; utakutana na changamoto nyingi lakini Roho Mtakatifu atakuwa anakufundisha namna ya kujibu, pia atakupa maarifa ya namna ya kuufikisha ujumbe wa Mungu mahali husika. Utajikuta hofu, woga, pamoja na aibu zinatoweka kabisa. Hauwezi kufanya kazi ya Mungu bila kuwa na Roho Mtakatifu; Ndio maana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba:
“…nawaleteta juu yenu ahadi ya Baba Yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.” – LUKA 24:49.
Hapo Yesu anasema: “...KAENI humu mjini, hata MVIKWE UWEZO utokao juu.” Roho Mtakatifu ndiye atupaye UWEZO / NGUVU ya kuitenda kazi ya Mungu.
NNE:
Utaweza kushinda vita vyote dhidi ya Shetani na jeshi lake. Bwana Yesu ametupatia AMRI ya kuharibu kila kazi ya Shetani wala hakuna lo lote litakalotudhuru (Luka 10:19). Tunaziharibu kazi hizo za Shetani kwa kutumia NGUVU na UWEZO wa Roho Mtakatifu anayekaa ndani yetu.
Hivyo ndivyo namna ya kujua kwamba wewe unaye Roho Mtakatifu ndani yako. Nakutakia amani na Baraka tele.
Kila mwanafunzi wa Yesu ni lazima awe na Roho Mtakatifu ~ (WARUMI 8:9).
Pokea Roho Mtakatifu katika jina la Yesu Kristo. Amina.
Majibu mazuri, kwa kuongezea uzito kufahamu jinsi Roho mtakatifu anavyokuja juu ya mtu bofya link hii >>> https://wingulamashahidi.org/2019/08/15/jinsi-roho-mtakatifu-anavyokuja-juu-ya-mtu/
ReplyDeleteAmen,nimebarikiwa na somo
ReplyDeleteAsante Sana nilikua nikiandaa somo nimepata pa kuanzia Barikiwa sana
ReplyDeleteNimefurahi sana juu ya kunifafanulia uwepo was roho mtakatifu Asante sana mtumishi
ReplyDeleteAmen
ReplyDelete