Yohana 3: 16-17 “Kwa maana jinsi hii
Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma
Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika
yeye.”
Mungu anakupenda sana, anajua jinsi unavyoenenda na amemtuma Mwana
wake wa pekee, Yesu afe msalabani kwa ajili ya ukombozi wako. Haupaswi
tena kuendelea kuishi dhambini, neema ya wokovu imefunuliwa na
yapatikana bure kwa kumkiri na kumwamini Yesu.
Warumi 10: 9-10 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa
kinywa chako yakuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu
alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata
kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”
Amua leo kumpa Yesu maisha yako upate tumaini jipya la uzima wa
milele. Ukimpokea Yesu utapata furaha, amani na uzima wa kweli. Huwezi
kuzipata baraka za Mungu kama hauna ushirika naye, na pia huwezi
kushinda dhambi bila msaada wa Mungu. Kama upo tayari kumpa Yesu maisha
yako, sali sala hii kwa kumaanisha kutoka moyoni.
“BWANA Yesu, nakuja mbele zako mimi ni mwenye dhambi. Nimetambua
makosa yangu na kuwa siwezi peke yangu. Naomba uingie ndani ya moyo
wangu, uondoe kiu ya dhambi, unisamehe makosa yangu yote, ufute jina
langu kwenye kitabu cha mauti, na uliandike kwenye kitabu cha uzima.
Nimeamua kukufuata wewe na kujitoa kwako siku zote za maisha yangu.
Nisaidie niweze kutembea nawewe daima.”
Hongera! Sasa umeokoka. Tafuta kanisa linalohubiri kweli ya neno la
Mungu uwe mshirika hapo. Jifunze biblia na omba kujazwa nguvu za Roho
Mtakatifu.
Post a Comment