0

Mazoezi ni muhimu kwa afya, kuna mazoezi ya aina mbalimbali. Unaweza kufanya mazoezi ya viungo au sehemu ya mwili kama tumbo, miguu, mikono, mgongo n.k. Vilevile kuna mazoezi ya kuchangamsha na kupasha mwili mfano mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba na mengineyo. 

Licha ya kuwa unaweza kutumia muda kidogo kufanya mazoezi kwa takribani dakika (30-45) kwa siku iwe asubuhi au jioni, mazoezi yana faida nyingi kiafya. 

Angalia video ya hapo chini inaonyesha namna ya kufanya mazoezi mepesi kwa dakika 10 nyumbani kwako bila kutumia vifaa. 

Soma hizi faida 17 za kufanya mazoezi uboreshe afya na maisha yako.

1. Mazoezi hukufanya uchangamke na kuwa shupavu.

2. Mazoezi huboresha ufahamu wako, uwezo wa kuelewa na kufikiri mambo katika mazingira yanayokuzunguka.

Kujua zaidi: Soma Namna ya kutunza afya ya akili na mwili wako 

3. Mazoezi huboresha uwezo wa ubongo kuhifadhi kumbukumbu. 

4. Mazoezi hupunguza msongo wa mawazo.

Soma pia: Namna ya kupunguza msongo wa mawazo 

5. Mazoezi huimarisha moyo hivyo huepusha maradhi yatokanayo na mapigo mabaya ya moyo. (Body exercise prevents and reduces cadiovasicular diseases)

6. Mazoezi humfanya mtu ajiamini kwa kupunguza stress, tension, wasiwasi n.k

7. Mazoezi hupasha mwili joto hivyo husaidia kuzuia na kupunguza baridi.

8. Mazoezi husaidia kuweka sawa kiwango cha cholesterol na mafuta yaliyopo mwilini. (Physical exercise burn more calories)

9. Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa kisukari.

Kujua zaidi: Soma hapa Ufahamu ugonjwa wa kisukari (diabetes)

10. Mazoezi hushusha kupanda kwa shinikizo la damu. (high blood pressure)

11. Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata baadhi ya maradhi ya saratani.(Reduces risk of getting breast cancer and colon cancer)

12. Mazoezi humsaidia mtu kuondokana na baadhi ya matatizo ya akili.

13. Mazoezi huongeza hamu ya mtu kutaka kula.

14. Mazoezi hupunguza uzito wa ziada wa mwili na kufanya mwili wako kuwa mwepesi.

Unaweza soma pia: Njia 5 za kupunguza uzito wa mwili 

15. Mazoezi huimarisha mifupa hivyo hupunguza matatizo yatokanayo na kudhohofika kwa mifupa jina la kitaalamu (osteoporosis)

16. Mazoezi huboresha kinga ya mwili.

17. Mazoezi husaidia kuweka sawasawa mifumo mbalimbali ya mwili. Mfano:mfumo wa ufahamu, mzunguko wa damu, homoni na misuli.

Hizi ni baadhi ya faida za kufanya mazoezi, yote ya yote mazoezi hurefusha maisha kwa kukufanya uwe mwenye afya njema. Ni vyema ukajiuliza, hivi ni kweli kufanya mazoezi na kula vizuri (vyakula bora) ni kuboresha maisha yako? Jibu ni NDIYO mazoezi na vyakula ni dawa pekee ya kutibu au kukuepusha na magonjwa mengi yanayoweza kuzuilika. Fanya mazoezi kuimarisha afya yako!

Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na makala hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top