0

 

 
Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamewavamia na kuwajeruhi askari mwenye no G369 PC Mansour na Hv507 PC Mwalimu, wakiwa doria ya pikipiki ambao walinyang'anywa silaha mbili aina ya SMG no 14301230 na 14303545 na watu wasio julikana mkoani Tanga.

Taarifa ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari imesema tukio hilo limetokea Januari 26, 2015 majira ya saa 23:30hrs eneo la barabara 04 jijini humo.

Aidha, imesema mmoja wa majeuhi askari mmoja no H 507 PC Mansour amejeruhiwa vibaya maeneo mbalimbali ya mwili na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Bombo.

Post a Comment

 
Top